@mwigulunchemba1 · 아프리카
이스라엘국은 아프리카 섹션의 탄자니아 관련 정부·공공업무 보도를 위해 므위굴루 은쳄바를 팔로우합니다.
Umekuwa wakati wenye tija na manufaa makubwa kwa nchi zetu mbili wakati wa ziara yako nchini, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Kenya, Dkt. William Samoei Ruto. Hotuba zenu Ikulu, Dar es Salaam, yako pamoja na ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mei 4, 2026, pamoja na mazungumzo yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), zimeonesha dhamira ya dhati ya kuimarisha ushirikiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Kenya, sambamba na kuendeleza maono ya waasisi wetu, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Mzee Jomo Kenyatta. Aidha, hotuba yako mbele ya Bunge imeakisi kwa dhahiri msimamo wa uongozi unaoamini katika mshikamano wa bara la Afrika na umuhimu wa ushirikiano wa kikanda kama nguzo ya kujenga uchumi imara na kujitegemea. Kama ilivyoelezwa na Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kuthamini na kuunga mkono juhudi hizi kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kindugu na kukuza ustawi wa wananchi wa nchi zetu mbili pamoja na ukanda mzima wa Afrika Mashariki. Karibu sana, na karibu tena Tanzania, Mheshimiwa Rais Dkt. William Samoei Ruto.
요청한 작업을 완료하지 못했습니다. 연결을 확인한 뒤 다시 시도해 주세요.